The House of Favourite Newspapers

Kanye West Ajipendekeza Filamu ya Deadpool 3

Kanye West

MKALI wa Muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Kanye West ameamua kufunguka ya moyoni kuwa angependa nyimbo zake zitumike kwenye filamu mpya ya Deadpool 3.

 

Kanye West (41) ambaye ni shabiki namba moja wa staa wa filamu hizo, Ryan Reynold, alitumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea hisia zake kuwa amekuwa akifuatilia Filamu za Deadpool tangu sehemu ya kwanza na kwamba angependa muandaaji atumie nyimbo zake kwenye Deadpool ijayo.

 

“Nazipenda Deadpool zote,” aliandika Kanye.“Nimesikiliza nyimbo nyingi kwenye filamu za Deadpool na kuona kama zinaendana na nyimbo ninazofanya, nipo tayari mzitumie.” Deadpool 2 imetumia baadhi ya nyimbo za Celine Dion ikiwemo Ashes huenda Kanye akafikiriwa kwa filamu ijayo

NEW YORK, Marekani

Comments are closed.