The House of Favourite Newspapers

WALID ‘WA PATORANKING’ APAGAWISHA ‘USIKU WA KUSI’ DAR LIVE -VIDEO

Walid (kulia jukwaani) akiwachombeza mashabiki wake wakati akipiga shoo katika Usiku wa Kusi Dar Live usiku wa kuamkia leo.

 

MSANII Walid Ali jana amefanya shoo yake ya kwanza nchini Tanzania katika Ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live katika sikukuu ya Idd Pili ambapo alimsindikiza mwanamuziki maarufu wa WCB, Harmonize, katika shoo iliyopewa jina la ‘Usiku wa Kusi’ ambapo baadaye pia aliibuka staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.

…Akiendeleza makamuzi.

Walidi aliimba wimbo wake wa ‘Namna Gani’ ambao amemshirikisha Patoranking wa Nigeria ambapo mashabiki waliojaa ukumbini hapo walilipuKa kwa furaha kubwa kutokana na umahiri wake wa kuimba kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Msanii huyo anayeishi nchini Uholanzi na ambaye kwa sasa yuko nchini hapa ambapo ni nyumbani kwao, amesainiwa katika lebo ya Patoranking.

Comments are closed.