Kaseja: Sijawahi Kufundishwa Kudaka Penalti – Video

MLINDA mlango wa timu ya taifa (Taifa  Star), Juma Kaseja, amesema kuzuia mikwaju ya penalti dhidi ya timu ya Burundi (kwa mbao 3-1) katika kinyang’anyiro cha kuwania kwenda Kombe la Dunia huko Qatar mwaka 2022 ni uwezo wake wa asili na hakufundishwa na mtu yeyote.

 

Kaseja amesema hajawahi kufundishwa jinsi ya kudaka penati lakini kikubwa amekuwa akifanya mazoezi na zaidi ni kipaji alichobarikiwa ndicho kinamfanya awe hivyo.

 

Kwa upande wa Tanzania, mfunguzi alikuwa ni Erasto Nyoni kisha Himid Mao na msumari wa mwisho ukapachikwa na Gadiel Michael.

 

Tanzania inasonga mbele kwenye hatua ya makundi kwa ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilika kwa kufungana bao 1-1 ambapo pambano la awali   timu zote zilitoka sare ya mabao 1-1.

 

MSIKIE KASEJA AKIFUNGUKA


Loading...

Toa comment