The House of Favourite Newspapers

Kaseke Amtaja Anayetaka Kucheza Naye Yanga SC

0

KIUNGO wa Yanga, Deus Kaseke, amesema kuwa kama kocha wa timu hiyo, Cedric Kaze ataendelea kumpanga
sambamba na mshambuliaji Yacouba Songne, basi atakuwa anafunga kwenye kila mchezo kwa sababu uelewano wao wakiwa dimbani ni wa hali ya juu sana.

 

Kaseke amefunguka kwamba, yeye na Yacouba wamekuwa wakielewana hata mazoezini na ndiyo maana kwenye mechi za hivi karibuni uswahiba wao uwanjani umekuwa ukinoga na imekuwa msaada kwa timu hiyo kupata pointi sita dhidi ya Azam FC na JKT Tanzania.

 

Katika michezo hiyo, Kaseke alifunga mabao mawili ambayo yote yametokana na pasi zaYacouba. “Mimi na Yacouba tumekuwa tukielewana hata tunapokuwa mazoezini, nishafahamu anacheza kwa mtindo gani, hata na yeye pia
anafahamu mimi nachezaje, ndiyo maana mara nyingi mipira anayoshika inatoka kwangu, na mimi nikipata mpira kwenye eneo la hatari, mara nyingi huwa inatoka kwake.

 

“Naamini kama mwalimu atazidi kutupa nafasi zaidi, nitakuwa nafunga au kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambayo yatatupa pointi ambazo sisi tunazihitaji kwa ajili ya kuwania ubingwa msimu huu,” alisema Kaseke Kaseke ambaye katika mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania aling’ara, alichaguliwa na mashabiki wa Yanga kuwa nyota wa mchezo huo.

 

Kaseke ameshinda tuzo hiyo kwa kuwashinda beki wa kushoto, Yassin Mustafa na kiungo mshambuliaji, Mkongomani Tuisila Kisinda baada ya kupata kura asilimia 65.

ISSA LIPONDA NA WILBERT MOLANDI.

Leave A Reply