The House of Favourite Newspapers

Watatu Wafa Maji Ziwa Victoria

0

WATU watatu wakazi wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu ambao ni wavuvi katika Ziwa Victoria, wamekufa maji kwa kuzama baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia katika shughuli zao kupasuka na kuingiza maji.

 

Tukio hilo limetokea jana Novemba  29, 2020,   katika kata ya Kabita tarafa ya Busega wakati wavuvi hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao za uvuvi kama kawaida.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa taarifa ya daktari aliyechunguza miili hiyo, kifo cha watu hao kilitokana na kunywa maji mengi na kukosa hewa na aliwataja kuwa ni Mnaga Manyama (umri wa miaka 28), Kulwa Juma (15) na Bitulo Manyama, wote wakazi wa Kabita wilayani Busega.

 

 

Abwao pia alitoa wito kwa wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi kufanya ukaguzi na matengenezo hitajika ya vifaa vyao mara kwa mara.

Leave A Reply