testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kata 21 Buchosa kushiriki Shigongo Jimbo Cup

0

Yale mashindano pendwa ya soka Kwa wananchi wa Jimbo la Buchosa chini ya uongozi wa Mbunge Eric Shigongo tayari mipira 25 yenye thamani shilingi 1,750,000 imesambazwa kata zote za buchosa.

Ugawaji wa mipira hiyo ni ishara ya kuanza maandalizi ya kuandaa timu za kata ambazo zitashiriki mashindano ya Shigongo Jimbo cup yanayotarajiwa kuanza  mwezi wa Julai  mwaka huu.

Katibu wa Mbunge Jimbo la Buchosa Julias Butogwa amesema kamati ya maandalizi imeamua kutoa mpira mmoja Kwa Kila kata na kata ya nyehunge, kalebezo, bupandwa na Bulyeheke zimepatiwa mipira miwili Kila kata Ili waweze kuunda timu za kata zenye ushindani.

Butogwa amewaomba viongozi wa chama katika kata husika washirikiane vyema na watendaji wa kata,vijiji pamoja na madiwani katika kuunda timu ya kata Ili waweze kupata timu nzuri.

“Tunawaomba viongozi wa chama kata husika mshirikiane Kwa pamoja na watendaji wa kata na vijiji pamoja na madiwani katika kuandaa timu zenu tunahitaji kupata wachezaji wazuri wenye vipaji kutoka Kila Kijiji kilichopo kwenye kata zenu,
Mbunge anapenda michezo na anahitaji vijana wacheze mpira Ili kumuunga mkono RAIS Dkt. Samia kuendeleza michezo nchini”.

Baadhi ya viongozi wa chama wamesema zoezi Hilo ni zuri na wanakaaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha Ili mashindano hayo yaweze kufanikiwa.

 

Leave A Reply