The House of Favourite Newspapers

Katambi: Ukiajiriwa Huwezi Kufikia Ndoto za Kuwa Tajiri

0

NAIBU Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Patrobas Katambi ametoa wito kwa vijana kutumia ujuzi walionao kufanya kazi mbalimbali badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

 

Katambi alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu alipotembelea ofisi za Global Group na kufanya mahojiano kwenye studio za +255Global Radio, kuhusu masuala mbalimbali yanayuhusu serikali kwenye wizara yake Machi 10, 2021.

 

Alisema kazi zipo nyingi lakini hazihitaji elimu badala yake kijana anatakiwa kuwa na maarifa na ujuzi.“Watu wengi waliofanikiwa ni wanaofanya kazi na si ajira.

Ukiwa na ajira huwezi kufikia ndoto za kuwa tajiri.“Ajira unakuwa mtumishi, maana yake unakuwa mtumwa. Nafasi hizi tunazozitumikia ni kwa neema tu ya Rais John Magufuli, hatupaswi kuwa wanafiki lazima tuwaambie vijana ukweli,” alisema Alisema wadhifa alioupata sio kwamba yeye ni bora sana kuliko wengine, bali huo ni mpango wa Mungu.

 

“Wajibu wangu ni kwenda kubadilisha maisha ya vijana. Mwaka 2015, Rais Magufuli aliahidi ajira milioni nane, zikapatikana ajira zaidi ya milioni 11.

 

“Rais aliagiza pesa zinazokusanywa kwenye Halmashauri, 4% iende kwa vijana, 4% iende kwa wanawake na 2% iende kwa wenye walemavu, mpaka sasa Serikali inawadai zaidi vijana mabilioni ya pesa ambayo imepeleka kule ili ziwasaidie kujiendeleza.“

 

Nimefikiria badala ya kuwapa pesa, vijana tuwape vifaa nusu na nusu tuwape pesa, mfano wanataka kuanzisha studio tutawalipia pango, kuwanunulia vifaa na nusu tutawapa pesa ya uendeshaji, hata wakishindwa vifaa vitaidia wengine, ukiwapa pesa tu zinaishia mfukoni.

 

“Lazima mwaka huu tukae kikao cha ‘Utatu Mtakatifu’ yaani Serikali, Waajiri na Wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi na waajiri wana siri nzito kila mmoja, tunataka tuzijue, Waziri wa Elimu naye awepo huenda vyuo vinatoa vyeti bila kujua soko la ajira linataka nini,” alisema Katambi.

STORI; Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply