The House of Favourite Newspapers

Kati ya Umeme na Maji Bora Nini?

0
 
Msanii Jay Moe aliwahi kuwauliza mashabiki wake katika moja ya ngoma yake “Kati ya mvua na Jua Bora Nini?”
 
Wakawa wanamchanganya wengine wakasema bora Mvua wengine bora Jua. 
Sasa waulize wakazi wa Dar Es Salaam kati ya Joto, Maji na Umeme bora nini?
 
Bila shaka na wewe watakuchanganya maana kila kona vilio, Joto kama lote, umeme hakuna, maji ndiyo usiseme ni mwendo wa mgao.
 
Shangaa sasa, watalaam wanasema kipindi hiki cha Joto kunywa maji mengi, maji hakuna.
 
Wakati huu wa Joto poza joto kwa kiyoyozi na feni na maji baridi, umeme hakuna.
Umeona mambo yanavyochanganya ndiyo maana kila mahali ukipita utasikia vilio “Rais Wetu, Mama Samia Suluhu uko wapi, tusaidie wanao.”
 
Basi kama na wewe unakabiliwa na matatizo haya matatu hebu paza sauti yako ya kilio kwa mama umwambie kati ya maji, umeme na joto unapenda nini?
 
Na @manyota_rich
Leave A Reply