The House of Favourite Newspapers

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo Awasili Simiyu kwa Ziara ya Kikazi

0
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM) Daniel Chongolo amewasili leo Mkoani Simiyu akitokea Mkoani Shinyanga kuanza rasmi ziara yake ya siku nne Mkoani humo.

Katibu Mkuu huyo katika ziara yake, atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa na serikali ikiwa pamoja na kuangalia uhai wa Chama hicho ndani ya mkoa.

Chongolo yupo Simiyu katika ziara ya kikazi ambapo atakagua Miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo

Katika Mapokezo ya kiongozi huyo, Viongozi mbalimbali was mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa David Kafulila, wakiwemo wabunge wa Mkoa huo wameshiriki mapokezi ya kiongozi huyo.

Leave A Reply