The House of Favourite Newspapers

Hukumu ya Sabaya Yaahirishwa Kutolewa Juni 10, Wakili Wake Afunguka – Video

0
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Hukumu ya Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake imeahirishwa hadi Juni 10, 2022

Ni kutokana na Hakimu aliyepangwa kuisikiliza kuwa nje ya Mkoa kikazi. Hukumu hiyo ilikuwa itolewe leo Jumanne, Mei 31, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

 

HUKUMU ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake sita, ilitarajiwa kutolewa hii leo Mei 31, 2022, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Katika kesi ya kwanza Sabaya na wenzake wawili walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari zilizojitokeza katika mwenendo wa kesi ya msingi katika mahakama ya chini.

Leave A Reply