The House of Favourite Newspapers

Kauli Tata Za Mwisho Za Ndikumana

0
Hamad Ndikumana enzi za uhai wake.

 

KIFO hakina huruma na ni fumbo kubwa kwa binadamu kwani hakuna ajuaye siku yake ya kuondoka duniani! Usiku wa kuamkia Jumatano (jana) ni siku ambayo haitasahaulika kwa familia ya aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Rayon Sports ya Rwanda ambaye amewahi kuwa mume wa mwigizaji Irene Uwoya kabla ya kutengana, Hamad Ndikumana baada ya kumpoteza mpendwa wao huyo.

 

Siku chache kabla ya kufikwa na umauti ambao kwa taarifa za awali inadaiwa kwamba ulitokana na matatizo ya moyo ambayo alikuwa hajawahi kuyagundua hapo awali, Ndikumana alikuwa akitoa kauli mbalimbali ambazo kwa sasa zinatafsiriwa kama alikuwa akijua kitakachotokea.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Ndikumana mara kadhaa aliandika ujumbe ‘tata’ kabla ya kifo chake, ukiwemo aliokuwa akimwandikia mzazi mwenzake, Uwoya kama ifuatavyo:

Hamad Ndikumana (kushoto ) akifanya yake enzi za uhai wake.

“Ungekuwa na roho ya kibinadamu ungekuwa hata unataka niwasiliane na mtoto ila miaka miwili hujawahi kuchukua simu unipigie umpe mtoto niongee naye hata picha tu hutaki kunitumia lakini naelewa kwa nini unafanya hivyo na baada ya yote haya naamini hutataka nimuone tena lakini sawa, Mungu yupo na ipo siku.

 

Irene ulichoniambia umeota juzi hujakosea hata kidogo ni kwa vile ulinifundisha mengi ndiyo maana hayaonekani na siwezi kuyaonesha lakini ndoto yako hujakosea nadhani nilikwambia mpaka umeniota labda nataka kufa na nikifa wala usihangaike Krish na Baasit kipo nilichowaandalia kwa siku zijazo na namuamini sana anachokisimamia wakati nitakuwa nimeondoka atatekeleza vizuri sana.

 

Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe sina pingamizi lolote tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria.” “Naisoma message ya mama ikisema, baba wala usihuzunike ulikuwa umepotea njia na yanayokukuta ndiyo njia sahihi Mungu aliona apitie ili akuokoe ipo siku utamshukuru na utaipata furaha uliyoipoteza na wala usijutie, kweli leo nimeamini maneno yako mama tabasamu limerudi kama zamani.”

 

Kipindi kimoja mama kaniambia: “Duniani utakutana na aina mbili za wanawake; wa kwanza atakupa maisha unayoyataka, wa pili atakupa mapenzi unayoyatamani. Ukiwa mmoja kati ya wenye bahati utampata atakayekupa vyote kwa pamoja, ukijikuta kwenye hali ya kuchagua basi chagua atakayekupa mapenzi. Namshukuru Mungu kwa sasa mimi ni mmoja kati ya wenye bahati. Asante mama kwa ushauri wako mzuri.”

Leave A Reply