The House of Favourite Newspapers

Kauli Ya Jakaya Kikwete Kwa Wanaotumia Mitandaoni Kupotosha

Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameamua kujibu kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni.

 

Usiku wa kuamkia leo, kupitia akaunti yake ya Twitter, Kikwete aliandika masikitiko yake juu ya namna watu wanavyotumia picha zake na kupotosha yale aliyoyasema juzi akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  ili kufanikisha matwaka yao ya kisiasa.
 
 

Aidha, Kikwete aliwataka watu hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa kupumzika. 
 
Kikwete pia alikanusha tuhuma za kuwa  ana tofauti na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa anamuunga mkono na serikali yake.
 
Kauli ya Kikwete ambayo imekuwa ikipotoshwa mtandaoni ni ile aliyoitoa kwenye  maadhimisho ya miaka 55 ya chuo kikuu hicho ambapo aliwataka  viongozi wapya kuenzi mazuri ya nyuma akimaanisha kwamba hivi sasa yeye ndiye Mkuu wa Chuo hicho (Chancellor), hivyo  akaahidi kuyaenzi mazuri aliyoyakuta kutoka kwa watangulizi wake.
 
“Ukiwa mpya lazima watu waone una mambo mapya, lakini mapya ya maendeleo,” alisema Kikwete na kuongeza: “Siyo mapya ya kubomoa ya kule tulikotoka,”

Comments are closed.