The House of Favourite Newspapers

Zair Atumia Watoto Kumvuta Mondi Geto!

0

ZARINAH Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ni mwanamama mrembo. Ni mfanyabiashara mwenye makazi yake pale Durban, Afrika Kusini.

Zari ni mama wa watoto watano. Watatu amezaa na aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Semwanga. Na wawili ambao ni Tiffah na Nillan amezaa na mwanamuziki mkubwa barani Afrika na C.E.O wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Miaka mitano nyuma, Zari na Diamond au Mondi walikuwa kwenye mahaba motomoto na kujaaliwa watoto hao wawili kabla ya kuachana kwao na kila mtu kushika hamsini zake tangu siku ile ya Valentine ya Februari 14, 2018.

Kuna tetesi kuwa mambo yamerudi kama zamani ingawa bado haijawa ‘ofisho’.

Zari ni mkwe ambaye hajawahi kuzungumziwa vibaya na mama mzazi wa Mondi, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’.

Zari naye aliwahi kukiri kuwa Mama Dangote ‘Kubwa la Maadui’ ni mtu mzuri kwani hajawahi kumzungumzia vibaya.

Zari na Mondi bado wanapendana kutokana na yale yanayoendelea kwenye maisha yao. Ni hivi juzi tu, Mondi alimuongezea Zari pesa kwa ajili ya kununua gari la kifahari aina ya Bentley, ishu ambayo inafanya zionekane ishara kuwa na uwezekano kuwa wamerudiana.

Baada ya kutengana kwao, kulikuwa na viposti vya hapa na pale kwenye sosho midia na kutumiana vimeseji pamoja na kwamba tuhuma kubwa iliyomng’oa jamaa huyo kwa Zari, ni kuchepuka na mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto wa kiume aitwaye Abdul Nasibu ‘Dyllan’.

Baadaye mawasiliano yalikatika zaidi baada ya Mondi kuwa na Tanasha Donna ambaye amezaa naye mtoto wa kiume aitwaye Naseeb Junior.

Lakini baada ya penzi la Mondi na Tanasha kuzima kama mshumaa, sasa mambo yanaanza kurudi taratibu.

Tukirudi kwa watoto, mara nyingi Tiffah anaonekana akiwa anazungumza na baba (Mondi) na bibi yake (Mama Dangote).

Zari amekuwa akiposti video za Tiffah na Nillan wakicheza nyimbo za baba yao.

Mfano ni baada ya kutoka Video ya Quranteen, Mondi aliposti kipande cha video (clip) ya Tiffah akiwa anacheza ngoma hiyo.

Sote tunajua kabisa mtoto anafundishwa, maana hawezi kujua yote hayo, hivyo mara nyingi Tiffah amekuwa akifundishwa na mama yake kuwa baba yake ni mwanamuziki na ndiyo sababu amekuwa akiposti video, akiimba na kucheza nyimbo za baba yake.

Si kitu kibaya kwa mama kumuelekeza mtoto kuhusiana na baba yake, ila inakuwa ni kama sababu ya Zari ‘kumvuta tena Mondi geto’ ili wawe pamoja kama zamani.

Tunajua hata Mama Dangote na familia nzima, wamekuwa wakitamani Zari arudi kwa Mondi japokuwa Zari amekuwa akiweka ugumu kurudi kwa jamaa, ila kwa sasa yeye mwenyewe ameanza kulegeza na kusemekana anafanya mbinu za kisayansi kumnasa tena jamaa huyo.

Kumekuwa na maneno kuwa Zari amekuwa akiwatumia watoto wake aliozaa na Mondi yaani Tiffah na Nillan kama njia ya kuwa karibu na baba yao Mondi.

Hii inaweza ikawa ni kweli, kwani mara nyingi Zari anapomuhitaji Mondi, amekuwa akiwatumia Tiffah na Nillan, hata kwa mawasiliano tu.

Iliwahi kutokea ishu moja, Tiffah alikuwa akimlalamikia baba yake (Mondi), kuwa hajampigia simu kwa muda mrefu mpaka akawa analia. Hii inaonesha dhahiri kuwa, Zari anawapanga watoto maneno ya kumwambia baba yao ili yeye anufaike kwa namna moja au nyingine.

Juzikati Zari aliposti video ikionesha masofa ya ndani yakiwa yamechanwachanwa kwa visu, kazi ambayo ilifanywa na Nillan ambapo alimtaka Mondi kununua mengine.

Baada ya kuposti video hiyo, wafuasi wa Instagram wakaanza kutoa maneno kuwa si kwamba Zari hana uwezo wa kununua masofa mengine, bali ni njama ambayo ameitengeneza kumuita Mondi geto kiaina.

Zari aliwahi kufunguka kuwa ana muda mrefu ‘hamjui mwanaume’ na amekuwa singo kwa muda, hivyo inaweza ikawa ni sababu ya kumuita Mondi aende akafanye yake.

Video ya Nillan ilikuwa stori kubwa, kwani Zari aliruka ‘live’ kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anaongea na Nillan.

Katika maongezi hayo, Zari akawa anampiga mkwara Mondi na mama yake waende kumchukua Nillan kutokana na kitendo alichokifanya.

Ishu imeonekana ni namna ya kumpiga Mondi mzinga au kumshawishi kwenda nyumbani kwa Zari nchini Afrika Kusini.

Kitendo cha kumuita Mondi aende Afrika Kusini, kinaweza kuwa njia ya kutaka kupasha kiporo, maana tunajua Mondi atakapokwenda kuwaona watoto wake, hawezi kulala chumba cha wageni kama alivyokwenda mara ya mwisho au hotelini, lazima tu atalala chumba kimoja na Zari.

Kwa hili, Zari anaweza kuwini mipango yake, kwani Mondi ana upendo mkubwa kwa watoto wake hao wawili kiasi kwamba yuko tayari kwa lolote ilimradi awafurahishe wanawe. Subira yavuta heri!

Leave A Reply