The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Kauli ya Mbowe, Lema Kufuatia Taarifa ya Kifo Mzee Ndesamburo

0

DODOMA: KUFUATI kifo cha aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro na (Chadema), Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia leo baada ya kuzidiwa ghafla ofisini kwake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepokea kwa masikitiko taarifa za msiba wa muasisi huyo wa Chadema.

“Nimepokea kwa masikitiko sana taarifa za kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo. Amekuwa wa msaada mkubwa sana kwa chama, wabunge na  tulikuwa naye kwenye Vikao vya Baraza Kuu la chama ambavyo tulimaliza juzi.

“Jana akiwa mzima alimpigia simu Meya wa Arusha Kalist Lazaro ili ampatie rambirambi ya milioni 3.5 kwa wahanga 35 wa ajali ya Lucky Vincent. Meya alifika ofisini kwa Ndesamburo majira ya saa 4 asubuhi.

“Wakati mzee alipochukua kalamu kuandika cheki kwa ajili rambirambi hiyo, alilegea, akadondosha kalamu, kutokana na hali hiyo Meya aliamua kuita wasaidizi ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa KCMC ambapo baada ya kufikishwa hospitalini hapo, nusu saa baadaye madaktari walisema ameaga dunia.” Alisema Mbowe.

Leave A Reply