The House of Favourite Newspapers

Kavejuru, Simizi Waapishwa Kuwa Wabunge – Video

0

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amemwapisha Kavejuru Felix kuwa Mbunge wa Buhigwe, Bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu, Mei 24, 2021. Kavejuru alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Mei 16, 2021, kwa kupata kura 25,274 sawa na 83.3% ya kura zote.

 

Kavejuru anachukua nafasi ya ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Dkt. Philip Isdory Mpango ambaye aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mbunge wa Muhambwe Dkt. Florence Samizi, amekula kiapo cha kuitumikia nafasi hiyo mbele ya Spika wa Bunge Job Ndugai. Dkt. Samizi alishinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika Mei 16, 2021, kwa kura 23,441 sawa na 66% ya kura zote.

 

Dkt. Florence anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye alifariki dunia miezi michache iliyopita.

Leave A Reply