The House of Favourite Newspapers

Kaza buti, lala salama!

0

Nyumba-10

KATIKA soka, mashabiki wanasema muda wa lala salama, yaani wakati wa mchezo kikanuni unakaribia kwisha, hivyo mwamuzi anaweza kupuliza filimbi ya kumaliza pambano ‘time’ yoyote.

Nyumba-3Ndipo unapoona timu iliyo nyuma, wachezaji wake wanahaha kupeleka mashambulizi ili kama siyo kushinda, basi angalau wasawazishe. Huu ni muda ambao wachezaji huonesha uwezo wa ziada kuhakikisha wanapata matokeo ya kuridhisha.

Nyumba-4Hii haina tofauti na bahati nasibu hii ya shinda nyumba ambayo sasa imebakiza siku tu, baada ya miezi sita kukatika, ikimtafuta msomaji mmoja wa magazeti ya Global Publishers, atakayetangazwa kuwa mshindi wa droo kubwa itakayochezwa Alhamisi ijayo.

Nyumba-1Kama ambavyo mchezaji wa timu iliyoshindwa anavyopambana kwa nguvu muda huu wa mwisho, ndivyo pia msomaji mwenye ndoto za kushinda nyumba hii yenye thamani kubwa hapaswi kushangaa na kuridhika kwa kuponi alizonunua hadi sasa. Kama umemudu kufanya hivyo kwa miezi sita ni wazi kuwa siku hizi chache hutakiwi kukosa magazeti yako ya Risasi, Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda na Ijumaa.

Nyumba-12Kuponi ya ushindi bado ni siri aijuaye Mungu na kwa maana hiyo, wanunuzi wa magazeti ya wiki hii bado wana nafasi kubwa ya kuibuka washindi. Hujachelewa, nenda kanunue sasa nakala ya gazeti uwe mmoja wa wamiliki wa nyumba za kisasa, yenye samani ndani yake, iliyopo Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Nyumba-8Ni rahisi katika kuipata nyumba hii, ukinunua moja ya magazeti hayo kwa shilingi mia tano tu (isipokuwa la Ijumaa, linalouzwa shilingi elfu moja), kata kuponi iliyopo katika ukurasa wa pili, halafu ijaze kama ilivyoelekezwa na baada ya hapo, mtafute wakala wa magazeti ya Global Publishers umpatie au kama uko Dar, nenda moja kwa moja ofisini kwetu, Bamaga, Mwenge.

Nyumba-7Zipo simulizi nyingi zinazoonesha jinsi watu wengi walivyoweza kupata vitu vyenye thamani kubwa kwa kushiriki michezo ya kubahatisha kama huu, kwani unaweza kuona kama kitu hakiwezekani au kimepagwa, lakini ukweli ni kuwa wewe unayesoma hapa, unaweza kuibuka kuwa mshindi.

Mtu anapata kitu katika kujaribu, huwezi kufanikiwa chochote katika maisha bila kujaribu, ndivyo ambavyo wafanyabiashara wakubwa walivyofanya, walianza kufanya na hatimaye wakafanikiwa. Hata waliofanikiwa kupitia kilimo, walianza kwa kulima.

Huwezi kuwa mshindi wa nyumba hii kama hutajaribu kujaza kuponi na kutuma. Na ukituma nyingi zaidi unakuwa katika nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mshindi.

Leave A Reply