The House of Favourite Newspapers
gunners X

Keanu Reeves Ana siri kubwa ya utajiri kwako!

1

Keanu_Reeves_2014UNAPOZUNGUMZIA waigizaji wenye utajiri mkubwa duniani, basi jina la Mkanada, Keanu Reeves litakuwa miongoni mwao. Kwa watu wa filamu, watakuwa wanamfahamu jamaa huyo kwa sinema zake baab’kubwa kama Matrix Revolution, Knock Knock, The Man of Tai Chi na nyingine nyingi.

Reeves alizaliwa mwaka 1964 huko Beirut nchini Lebanon. Baba yake, Samuel Norwin Reeves alikuwa Mmarekani kutoka katika Visiwa vya Hawaii huku mama yake, Patricia Bond akiwa ni Mwingereza kutoka Essex.

Mama yake alikutana na baba yake alipokuwa nchini Lebanon kikazi. Baba yake alikwenda Lebanon katika harakati zake za kuuza madawa ya kulevya hivyo Reeves hakulelewa na baba yake ipasavyo kwani mzazi huyo alikamatwa huko Hawaii alipokuwa akisafirisha madawa ya kulevya.

Baada ya hapo, mama yake alikuwa akibadilisha wanaume. Ilikuwa leo akiolewa na huyu, kesho anaachika na anaolewa na mwingine.

Kwa kipindi cha miaka mingi aliishi nchini Canada hivyo kumfanya kuchukua uraia wa huko ila hadi sasa anaishi nchini Marekani huku akishikilia kadi yake ya Green ambayo inamfanya kuonekana pia ni raia nchini humo.

NI MTU WA WATU

Reeves amekuwa tofauti na mastaa wengine. Wapo mastaa ambao wamekuwa wakionekana kwa tabu mitaani, hawataki kuonekana mara kwa mara lakini jamaa huyu amekuwa hakauki mitaani.

Hupenda kujichanganya na watu wengi na alipoulizwa sababu ya kufanya hivyo anasema kwamba watu wanaonunua filamu zake ni haohao waliokuwa mitaani na kama akiisema ajifiche, basi atasababisha watu hao kutokumpenda.

NI MTOA MISAADA MZURI TU

Jambo la kuwasaidia watu wengine limekuwa si tatizo kwake. Amekuwa akitembea hospitali nyingi na kutoa misaada. Amekuwa akiwasaidia maskini wengi kwa kuwapelekea chakula mitaani, amekuwa akifanya hivyo mara nyingi.

Katika filamu zake za Matrix Reloaded na Revolution, jamaa alilipwa dola milioni 114 (zaidi ya Sh. bilioni 230) lakini akachukua dola milioni 80 (zaidi ya bilioni 160) na kuwasaidia maskini mitaani.

BABA WA WATOTO WATATU

Reeves ana watoto watatu, Kim Reeves, Karina Reeves na Emma Reeves ambao amezaa na mwanamke asiyependa kumuweka hadharani bila kuanika sababu ya kufanya hivyo.

UTAJIRI WAKE

Mpaka sasa, Reeves ana utajiri wa dola milioni 380 (karibia shilingi bilioni 800) ambao ameupata katika kazi zake za filamu na biashara zake nyingine.

TUNAJIFUNZA NINI?

Reeves anasema kinachompa utajiri ni kusaidia watu wengine, hajioni kuwa na kidogo cha kushindwa kuwasaidia watu wenye matatizo. Kila anapokuwa na semina ya kufundisha namna ya kufanikiwa, huwaambia watu kwamba siri ya kwanza kufanikiwa ni kuwasaidia wengine.

Kwako msomaji! Usiangalie una kiasi gani, inawezekana una kiasi kidogo lakini unaweza kuwasaidia wengine. Unapoanza kupata mafanikio. Pia kumbuka wale waliokuwa hawana kitu.

Imeandaliwa na Nyemo Chilongani kwa msaada wa mtandao.

1 Comment
  1. Masanja daudi says

    Ama kweli kusaidia watu bila kubagua njinsia kunamfanya mtu kubarikiwa na kupata mafankio makubwa mara mbili zaid ya ulichotoa!! Tujifunze kutoa misaada kwa wasio jweza!

Leave A Reply