The House of Favourite Newspapers

Aunt ammwagia mil. 6 Neema Chande!

0

aunty (5) Neema Chande akitabasamu.

STORI: Waandishi wetu, Wikienda

Dar es Salaam: Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemmwagia aliyewahi kuwa Miss Ruvuma, Neema Chande, minoti ya zaidi ya shilingi milioni sita na kusababisha minong’ono kuwa alizifuma wapi?

aunty (6)Aunt Ezekiel

Tukio hilo la kufuru ya aina yake lilijiri kwenye Ukumbi wa PJ uliopo Kinondoni, Dar ambapo Neema aliandaliwa Kibaokata cha kumuaga tayari kwa kuolewa wikiendi iliyopita.

aunty (3)Aunt Ezekiel na Neema Chande.

Hata hivyo, baadhi ya waliohoji sababu ya Aunt kutoa hela zote, mwenyewe aliwajibu kuwa alitoa mshiko huo kwa sababu ya urafiki walionao na Nice kwani si urafiki tu kwa sasa umekuwa undugu.

aunty (2)“Mimi na Nice (dada wa Neema Chande) ni ndugu sasa! Hivyo tulikuwa tukifanya sherehe ya mdogo wetu,” alisema Aunt.

Kwa upande wake Nice alimmwagia Neema zawadi kibao zikiwemo dhahabu zilizowatoa udenda waalikwa.

Leave A Reply