The House of Favourite Newspapers

Kemikali za Kutengeneza ‘Unga’ Zakamatwa Dar

0

Mamlaka ya Kupambana na Kuthibiti Madawa ya Kulevya ‘unga’, leo imekamata na kukagua kontena mbili zenye kemika zaidi ya lita 5,000 ambazo kama zikichepushwa zinaweza kutengeneza dawa za kulevya ‘unga’.

Operesheni hiyo imeongozwa na kamishna wa mamlaka hiyo, Rogers Siyanga na mamlaka zingine ambapo walivamia ofisi za AMI zilizopo Tabata jijini Dar ambao wanahusika na masuala ya mizigo.

Akizungumza na wanahabari, Kamishna Msaidizi wa Ukaguzi na Sayansi ya Jinai, Bertha Mamuya amesema kilichofanyika leo ni muendelezo wa oparesheni ambazo zimekuwa zikifanywa na mamlaka hiyo.

“Tulikuja kufanya uchunguzi kwenye hizi kontena mbili ambazo ni mali ya Kampuni ya Techno Net Scientific ya Kijitonyama, Dar. Tumebaini kuwemo kwa kikali zaidi ya lita 5,000 ambazo baadhi yake zikitumiwa vibaya zinaweza kutengeneza dawa za kulevya.

“Kama mamlaka, tutapeleka sampo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye atawasilisha kilichobainika,” alisema Mamuya.

Leave A Reply