The House of Favourite Newspapers

Kendall, Harry Styles wazua maswali

0

harry-styles_glmaour_21nov13_AKM-GSI_bbt_810x540Modo kiwango Kendall Jenner akiwa na mwanamuziki Harry Stayles.

CARIBBEAN, Mexico
BAADA ya wiki iliyopita kuonekana wakiwa pamoja kwenye mtoko wa chakula cha usiku, modo kiwango Kendall Jenner na mwanamuziki Harry Stayles wameonekana tena wakiwa katika mikao ya kimahaba kwenye boti huko Carribean.

Wawili hao ambao wanaripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi bado hawajazungumza lolote kuhusu hali iliyopo baina yao kwa sasa licha ya kuwa wamekuwa wakionekana kuwa kwenye mikao ya kimahaba.

kendall-jenner-harry-styles-23Katika sikukuu ya kuukaribisha mwaka mpya, Kendall ambaye ni mdogo wa modo wa kimataifa, Kim Kardashina na Harry ambaye ni memba wa Kundi la One Direction walionekana wakiwa pamoja kwenye boti katika Visiwa vya Caribbean wakila bata na marafiki zao.

Wawili hao awali waliripotiwa kutoka pamoja mwaka 2013 baada ya kuonekana wakiwa pamoja zaidi kama wapenzi kwenye mitoko mbalimbali hasa ya chakula cha usiku.

Hata hivyo Harry aliwahi kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikana na kusema imekuwa kawaida kwenda pamoja na Kendall ‘dinner’ lakini wao siyo wapenzi.

Leave A Reply