The House of Favourite Newspapers

Kendrich Lamar Kumkumbuka Prodigy BET

0
Kendrich Lamar

HUKU wanamuziki wawili, Havoc na Lil Kim wakiwa wamejitolea kumkumbuka rapa wa Kundi la Mobb Deep, Prodigy aliyefariki mapema wiki iliyopita, rapa mwingine, Kendrich Lamar amejitolea kumkumbuka mwanamuziki huyo wakati wa utoaji wa Tuzo za BET zitakazofanyika kesho (Jumanne) nchini Marekani.

Ikumbukwe kwamba mara baada ya Prodigy kufariki dunia, BET hawakuweka muda wa kumkumbuka staa huyo kwa kuogopa kuvuruga ratiba iliyokuwa imepangwa hivyo kutoa dakika moja tu, tena ya mwisho kumkumbuka Prodigy ambaye ana mchango mkubwa katika Muziki wa Rap nchini Marekani.

Prodigy

Mpaka leo bado taarifa haijatoka rasmi kuelezea kifo chake ingawa wengi wanadai kwamba mwanamuziki huyo aliyekuwa mgonjwa wa Sickle Cell alifariki kwa matumizi ya madawa ya kulevya.

Na Nyemo Chilongani.

Leave A Reply