The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Amtisha Rasta Aliyetaka Kutua Simba

0

KIUNGO wa Madini FC, Awesu Awesu ‘Rasta’, amefunguka kuwa amefuta mpango wake wa kujiunga na Simba baada uongozi wa timu hiyo kumbakisha kiungo wake Jonas Mkude na kumchukua aliyekuwa kiungo wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

 

Awesu ambaye alikuwa akitakiwa kujiunga na Simba baada ya kuonyesha kiwango kizuri walipocheza dhidi ya timu hiyo kwenye robo fainali ya Kombe la FA msimu uliopita, nafasi anayocheza ya kiungo wa kati, pia Niyonzima anaicheza.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Awesu alisema kuwa ni ngumu kwa sasa kwake kukubali kutua Simba kwa kuwa tayari imeshasajili wachezaji wakubwa zaidi yake ambao watamfanya aishie kukaa benchi ndani ya timu hiyo kitu ambacho hataki kimtokee.

 

“Unajua ni kweli nilikuwa na mipango ya kujiunga nao, siwezi kukataa hilo kwa sababu walinifuata kuzungumza nao ingawa kuna mambo madogomadogo tulikuwa hatujamalizana lakini nimeona kufuta mpango huo kwa sababu naona sitaweza kucheza Simba bali nitaishia kukaa benchi.

 

“Nasikia Mkude wamemuongeza mkataba halafu wameshamsajili Niyonzima, sasa mimi hapo nitacheza nafasi gani, Niyonzima anunuliwe kwa milioni 100, halafu kwangu hata nusu yake haijafika unadhani wenyewe watakubali akae benchi yeye au Mkude? Nitacheza ligi kuu lakini siyo kwenye timu hiyo wala Yanga,” alisema Awesu.

 

Ibrahim Mussa | Dar es Salaam

Leave A Reply