Kenya, Uganda na Tanzania Zawasilisha Maombi ya Kuandaa AFCON 2027
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepokea maombi kutoka nchi sita zinazowania uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ikiwemo Tanzania.
Jumla ya waombaji sita wamefanikiwa kuwasilisha maombi yao ambao ni Algeria, Botswana na Misri huku Kenya, Uganda na Tanzania zimewasilisha maombi ya kuandaa fainali hizo kwa pamoja.
Hatua inayofuata ni kuwasilisha zabuni ya mwisho ifikapo Mei 23, 2023 ikijumuisha nyaraka zote (makubaliano ya uenyeji, makubaliano ya miji mwenyeji, dhamana ya serikali, na nyinginezo).
Ukaguzi utaanza kufanyika Juni 1-15, 2023 na uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo utafanywa na Kamati ya Utendaji ya CAF.