The House of Favourite Newspapers

Kerr: Tutafuta machozi yetu kwa Stand

0

o7bkHdw7

Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr.

Mohammed Mdose,Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amewataka mashabiki wa Simba kusahau kipigo walichokipata kutoka kwa Yanga na kuwaahidi kuendelea kugawa dozi katika mechi zijazo wakianzia na ya leo Jumatano dhidi ya Stand United.

Simba ambayo Jumamosi iliyopita ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Yanga, inakutana na Stand United yenye kumbukumbu ya kuifunga JKT Ruvu bao 1-0 kwenye Uwanja wa Karume, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kerr alisema kuwa baada ya kupoteza mechi na Yanga, amewajenga wachezaji wake kisaikolojia na kuwafanya wawe na morali ya hali ya juu ya kuendelea kupambana katika mechi zijazo.

Alisema anawatoa hofu mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa timu yao bado ipo imara kwa kupambana kwenye mechi zilizobaki hivyo hakuna kukata tamaa, mapambano bado yanaendelea.

“Vijana wapo tayari kwenda kupambana, tumeshasahau yaliyopita, tumerekebisha makosa yetu, tunaenda kucheza na Stand kutafuta ushindi tu na siyo vinginevyo, nina imani tutashinda.

“Kupoteza mechi iliyopita hakuna maana kuwa ndiyo tumeshaishiwa, ukipiga hesabu utaona tumebakiwa na mechi kibao, tutaendeleza wimbi letu la ushindi mbele ya Stand,” alisema Kerr.

Leave A Reply