KESI IKIELEKEA UKINGONI, SCORPION AZIDI KUWA TISHIO

Kesi inayomkabili Mwalimu wa Sanaa ya Mapigano, Salum, Njwete ‘Scorpion’ ya katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar, ya kumshambulia na kumtoa macho, Kinyozi, Saidi Mrisho ikiwa inaelekea ukingoni, mshitakiwa huyo ameonekana kuzidi kuwa tishio baada ya leo kufikishwa mahakamani hapo peke yake akiwa kwenye gari maalum lenye bendera nyekundu inayoashiria hatari huku askari wanaomlinda wakiwa wameongezeka.

Tangu kuanzia kwa kesi hiyo hajawahi kufikishwa mahakamani hapo katika ulinzi kama huo hali inayoonesha askari wao wanahisia fulani na mshitakiwa huyo aliyejizolea umaarufu kwa utaalamu wa mapigano.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana Alhamisi ambapo upande wa mashitaka ukiwakilishwa na Koplo Bryson ulitakiwa kufunga ushahidi wake lakini Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Frola Haule aliiahirisha baada ya Wakili wa mshitakiwa huyo, Juma Nassoro kushindwa kufika mahakamani hapo ambapo inatarajiwa kuendelea kesho Ijumaa.

 

Ulinzi wa mshitakiwa uliendelea kuwa gumzo mahakamani hapo ambapo wengi walisikika wakiujadili ulinzi huo hasa wakati makomandoo wa Magereza walipokuwa wakiudandia gari hilo huku likiondoka na walivyoshuka kwa kuruka kabla gari halijasimama.

 

 

Na Richard Bukos/GPL

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment