The House of Favourite Newspapers

Kesi Kina Mdee: Dk. Lwaitama Asema Atatetea Uanachama Wao Wakiachia Ubunge

0

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof. Azavel Lwaitama, amesema atakuwa wa kwanza kuwatetea wabunge viti maalum 19, warejeshewe uanachama wao, endapo watakubali kutoka bungeni.

Akihojiwa maswali ya dodoso katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam na Wakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya, Machi 10, 2023, Prof. Lwaitama amedai kosa la wabunge hao ni kuingia bungeni jijini Dodoma kinyume cha sheria.

Mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, Prof. Lwaitama alidai ” hata leo hii wakitoka bungeni nitakuwa wa kwanza kuwatetea warudi kwenye chama.”

Baada ya kutoa kauli hiyo, Wakili Panya alimhoji iwapo shida ni bungeni ambapo Prof. Lwaitama alijibu akidai “utaratibu ni batili, wa kihuni wa kuingia bungeni. Mtu kaachiwa, katolewa gerezani usiku, ku- forge barua, hiyo ndiyo haitakiwi. Tunajenga taifa la namna gani? Hoja sio wao ni utaratibu.”

Prof. Lwaitama anahojiwa maswali hayo kuhusu hati zao za kiapo kinzani walizowasilisha mahakamani hapo kujibu Kesi Na. 36/2022, iliyofunguliwa na wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee.

Mdee na wenzake 18, wamefungua kesi hiyo wakipinga uamuzi wa Chadema kuwafukuza uanachama kwa madai kuwa haukuwa halali, ambapo wanaiomba mahakama ifanye mapitio dhidi ya mchakato uliotumika kuwafukuza Chadema.

Prof. Lwaitama anaendelea kuhojiwa maswali mahakamani hapo.

OFFICIAL NAI AANIKA MAISHA YAKE, KUPIGANA KAMA MANDONGA, AKWEPA KUMTAJA MPENZI WAKE |KONA YA MTAA

Leave A Reply