The House of Favourite Newspapers

Kesi Ya Akina Rugemalira na Singasinga Yaahirishwa

0

James Rugemalira (mwenye mvi) na mwenzake Harbinder  Singh Sethi wakifikishwa mahakani.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi maarufu kama ‘Singasinga’ na  mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.

 

Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya kutoka kortini.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

=====

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO MAHAKAMANI

Leave A Reply