The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Serikali Yatangaza Kutokomeza Homa ya Ini

0
Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na wanahabari leo.

SERIKALI imesema itaweka mikakati ya nguvu katika kudhibiti na kuutokomeza kabisa ugonjwa wa homa ya ini kulingana na Mpango Mkakati wa Kwanza uliowekwa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO) utakaoupiga vita ugonjwa huo kwa kipindi cha tangu mwaka 2016 hadi 2021.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alipokutanana waandishi wa habari leo na kuweka bayana kwamba ugonjwa huo ambao unachukua maisha ya Watanzania wengi kuliko Ukimwi, kulingana na utafiti, hivi sasa unawaathiri watu wanane kati ya 100 nchini.

 

“Utafiti umesema kwamba homa ya ini ni ugonjwa hatari ambapo Watanzania wanane kati ya mia moja wana vidudu vya ugonjwa na tatizo ni kwamba miongoni mwa walio na ugonjwa huo, huwa hawajui kwamba tayari wanao,” alisisitiza Mwalimu akisema mpango huu umedhamiria kuutokomeza kabisa ugonjwa huo nchini.

Leave A Reply