The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Aveva, ‘Kaburu’ Yasogezwa Mbele

0
Rais wa Simba, Evans Aveva (wa kwanza kushoto) na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa mahakani Kisutu.
…Wakiingia mahakani.
‘Kaburu’ akiongea jambo makamani hapo.

Kesi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’  leo imeendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo upande wa mashtaka umeieleza mahakama hiyo kwamba umekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi hivyo hivyo wanasubiri ripoti.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Estazia Willson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo aliiiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu.

Aidha hakimu aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha ripoti hiyo ya uchunguzi akisema kwamba watuhumiwa wako rumande hivyo si bora kesi hiyo kuahirishwa kila mara.

(HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

LIVE: Sakata la Nyumba 17,000 Kubomolewa, Makonda Aibukia Bonde la Msimbazi

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply