The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Madabida Kusambaza Dawa za ARVs Vuta Nikuvute Kortini

Madabida akiwa kortini.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa kesho Ijumaa, Deseaba 8, 2017 itatoa uamuzi kama mahakama hiyo inamamlaka ya kusikiliza Kesi ya uhujumu uchumi ama la inayomtuhumu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake watano waliofikishwa katika au la!

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Madabida na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ‘ ARV’s ‘ na kusababisha hasara ya Sh.Mil 148 ambayo ipo chini ya bilioni moja ambapo walifunguliwa kesi hiyo mpya namba 80 ya 2017, baada ya mahakama kuwafutia kesi kama hiyo iliyofunguliwa mwaka 2014.

 

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Seif Shamte (mkurugenzi  wa uendeshaji),  Simon Msoffe (meneja masoko) na  Fatma Shango (mhasibu msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd, Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa. ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kuisambazia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kopo 4476  za ARV.

 

Pia washtakiwa wanadaiwa kujipatia Dola za Marekani 98,506.08 (sawa na Sh 148,350,156 za Tanzania kwa udanganyifu baada ya kuonyesha kwamba fedha hizo ni malipo ya makopo 12252 ya dawa hizo za ARV’s.

 

Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na Wakili wa Serikali, Pius Hilla Wakati ambapo upande wa utetezi wa watuhumiwa wanawakilishwa mawakili Denis Msafiri, Makaki Masatu na Nehemiah Nkoko ambapo wakili wa utetezi, Msafiri alidai kuwa Mahakama ya Kisutu inayo mamlaka ya kuisikiliza hiyo kwa sababu kiwango chake cha fedha  kipo chini ya Sh.1 bilioni.

Kaburi la Mume wa Zari, IVAN DON, Lafukuliwa!

Comments are closed.