The House of Favourite Newspapers

‘Mpemba wa Magufuli’ Kupelekwa Mahakama ya Mafisadi

0
Yusuf Ally ‘Mpemba wa Magufuli’ (mwenye tisheti nyekundu) akiwa na wenzake walipofikishwa kortini leo.

HATI ya mashtaka ya kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo inayowakabili mfanyabiashara Yusuf Ally maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ inatarajiwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi).

Wakili wa Serikali, Elia Athanas amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba kuwa jalada la kesi hiyo limekamilika, hivyo wanaomba muda ili wapeleke hati ya mashtaka katika Mahakama ya Mafisadi.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 19, mwaka huu.

Wakiwa kwenye viunga vya mahakama.

Mbali ya Yusuf Alli, washtakiwa wengine ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa ambao wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Tsh. Milioni 785.6.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba 2015, wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Tsh Milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

 

LIVE: Aliyeibiwa Mtoto wa Miaka 2 Ampata Akiwa na Miaka 15!

Leave A Reply