Kesi ya Rugemalira, Seth Bado Sana – Video

KESI ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyabiashara wawili, Habinder Seth na James Rugemarila, upande wa mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

 

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisaidia na wakili kutoka Takukuru, Iman Nitume, ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa. Rugemalira na Seth wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

 

“Kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa” alidai Simon.


Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, mwaka huu, itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande. Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

 

Miongoni mwa mashtaka wanayokabiliwa nayo ni shtaka wanadaiwa kulitenda kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam la kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

 


Loading...

Toa comment