The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Rugemalira, Seth Yapigwa Kalenda Tena

0

KESI inayowakabili mfanyabiashara, James Rugemarila, na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya IPTL, Habinder Seth na mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege kwa pamoja wkikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi,  imeahirishwa hadi Januari 14, 2021, kutokana na hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa likizo.

 

Shauri hilo linasikilizwa na Hakimu Huruma Shaidi. Washtakiwa Seth na Rugemalira kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya  Dola za Marekani 22,198,544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.

 

Mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, mwaka 2017, kwa makosa hayo ambapo inadaiwa waliyatenda Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic Tawi la kati Kinondoni.

 

Leave A Reply