The House of Favourite Newspapers

KESI YA TIDO MHANDO YAAHIRISHWA HADI FEBRUARI 28

Tido Mhando akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.
…Akiwa na mmoja wa nguli wa utangazaji nchini na kimataifa, Charles Hillary (wa pili kulia).

 

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kuisababisha serikali hasara ya Sh, milioni 887 inayomkabili  aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando ambayo imeahirishwa  hadi Februari 28, mwaka huu.

 

 

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ruswa (Takukuru), Leonard Swai,  amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa, kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea  mtuhumiwa huyo  maelezo ya awali.

 

Hata hivyo, Wakili wa Mhando, Ramadhan Maleta,  ameieleza mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya awali (Ph) hivyo anaomba ahirisho.

 

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na ombi hilo.

 

Katika hati ya mashtaka Mhando anakabiliwa na makosa matano yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji  (TBC).

 

 

Comments are closed.