The House of Favourite Newspapers

Kessy aundiwa kamati

0

Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani.jpgHassan Kessy.

SIMBA imeona isiwe shida kwani imeunda kamati maalum ya kushughulikia usajili wa beki wake wa kulia, Hassan Kessy kuhakikisha anabaki kikosini.

Hatua hiyo ya Simba imekuja baada ya taarifa za beki huyo kutakiwa na Yanga kupamba moto huku akiwa anaelekea kubakiza miezi sita katika mkataba wake.

Uongozi wa Simba kupitia Rais Evans Aveva umesema utafanya mazungumzo na Kessy baada ya mchezo wa Taifa Stars na Algeria leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa kufuzu Kombe la Dunia 2018.
Kessy yumo kwenye kikosi cha Taifa Stars na ni mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Simba tangu alipojiunga nao msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aveva alisema wamemuacha beki huyo amalize majukumu ya timu ya taifa, baada hapo watazungumza naye kuhusu mkataba mpya.
Awali Simba ilisema ingekutana na Kessy baada ya kutoka kambini Afrika Kusini na Taifa Stars, lakini inaonekana mambo yamekuwa magumu na sasa wanasubiri kukutana baada ya mechi ya Algeria. “Kessy kwa sasa tumeamua kumuacha amalize majukumu ya timu ya taifa, baada ya hapo tutakutana naye kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mkataba,” alisema Aveva.
“Jambo la msingi ni kwamba, tutahakikisha kila kitu kinakwenda sawa ili Kessy abaki kikosini maana kama unavyojua mambo ya usajili huwa na presha kubwa.”

Leave A Reply