The House of Favourite Newspapers

KEVIN DURANT ANABADILI TU MADEMU

 CALIFORNIA, Marekani: NYOTA wa NBA, Kevin Durant, amezidi kwa warembo, kwani taarifa zinasema sasa anatoka na modo Sabrina Brazil.

Taarifa zinanyetisha kuwa mkali huyu wa timu ya Golden State Warriors amekuwa aki­toka na mrembo Sabri­na tangu alipotengana na mrembo mwingine, Cassandra Anderson.

 

KD, 30, pia ame­kuwa akihusishwa ki­mapenzi na mpenzi wa zamani wa Chris Brown, Amy Shehab pamoja na mwimbaji Keri Hilson. Durant alisitisha uhusiano wake na Cassandra, Oktoba, mwaka jana.

Lakini fowadi huyo pia aliachana na mchumba wake Moni­ca Wright mwaka 2014 kwa madai ya kush­angaza.

Alisema: “Nilikuwa na mchumba, la­kini sikujua jinsi ya kumpenda, unajua nin­achokisema? Tuliten­gana kwa staili hiyo.”

Lakini Monica, ambaye anach­eza kikapu kwenye Ligi ya Wanawake Marekani (WNBA), alitoa sababu tofauti akidai waliten­gana kwa saba­bu ya imani yake kali kwa Mungu.

 

Mrembo huyo alisema: “Nilikosolewa sana kuto­kana na hilo, lakini nadhani Mungu alikuwa upande wangu. Kwa sababu nil­ishikilia kile ambacho najua ni kweli, hicho ndicho Mungu atan­ituza badala ya kile ambacho watu duniani w a ­naamini ni kizuri.”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.