Huyu Ndo Demu wa Staa Anayependa Kukaa Uchi!
LONDON, England: MR EMBO Sarah Kohan ambaye ni mpenzi wa straika wa West Ham, Javier Hernandez ‘Chicharito’, amepiga picha akiwa uchi huku akiinadi mimba yake mpya.
Sarah ameshaeleza mara kadhaa kwamba kukaa uchi ndiyo furaha yake kubwa maishani. Sarah, 24, mwenye wafuasi milioni 1.3 kwenye Insta, amekuwa akitoka na Chicharito tangu mwaka jana, na tayari ameshanasa ujauzito ambao unaelezwa ni wa mwezi mmoja.
Raia huyo wa Australia ni msomi akiwa ni mhitimu wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Harvard. Sarah amekuwa akisisitiza kwamba kuwa uchi ni moja ya vitu anavyopenda zaidi maishani.
Hernandez ambaye ameifungia West Ham mabao matano katika michezo 16 aliyoichezea timu hiyo msimu huu, inaelezwa yupo mbioni kuondoka klabuni hapo mwezi huu huku Barcelona ikitajwa kumhitaji.
Comments are closed.