The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Khadija Kopa Afikisha Ujumbe Huu Kwa BASATA- (Video)

Mama wa mipashao Khadija Kopa ana jambo limemkaa rohoni kwa muda mrefu sana na angependa liwafikie wahusika. Global TV Online imekutana nae na kukufikishia hii exclisively kutoka kwake.

Malkia wa mipasho Tanzania Khadija Kopa hivi karibuni alikaa chini kupiga stori na camera za Global TV Online na kwenye mazungumzo yetu msanii huyo mkongwe wa muziki wa Taarab alifunguka jinsi ambavyo anaumizwa na mwenendo wa muziki huo nchini, kwa maneno yake; sisi tunaumiza vichwa sana lakini muziki wetu unapotea… akidai yote ni kutokana na BASATA kushindwa kufanya kazi yao ya kuwasimamia wasanii wa muziki wa Taarab ipasavyo.

BASATA wanatusajili sisi, tunalipa ada zetu kwa ajili ya BASATA lakini hawatusimamii. Sisi tunaumiza sana vichwa kwenye kazi hizi ila kuna watu wanaunda mabeni kwa ajili ya kupiga viingilio bia na nyimbo hizi hizi zetu… muziki wetu unapotea. Hivyo naona kama vile BASATA hawawezi kutusimamia maana tumeshaomba sana juu ya mambo haya lakini wameshindwa hivyo ninaiomba Serikali, Wizara na Waziri watusaidie kuhusu habari ya nyimbo zetu.” – Khadija Kopa.

Akaendelea kusema…

Mambo mengine wanafuatilia… utasikia mtu ametoa wimbo mbaya anafungiwa lakini mbona hawashughuliki kwa haya mambo mengine, mengine mbona hawafuatili? Sasa kuna haja gani ya kukaa Serikalini na kuchukua mishahara?” – Khadija Kopa.

Itazame interview nzima ya Mama wa Mipasho Khadija Kopa hapa chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Interview/Video Na: Becka Issa

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, muziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.