The House of Favourite Newspapers

Kibwana: Bado Sijafikia Kiwango Ninachokitaka

0

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Kibwana Shomari amesema kuwa bado hajafikia kiwango ambacho anakitaka kwa sasa jambo linalomfanya afikirie kufanya vizuri zaidi.

 

Kibwana aliibuka ndani ya Yanga msimu wa 2020/21 akitokea kikosi cha Mtibwa Sugar na amekuwa chaguo la kwanza la makocha ambao wanapita hapo tangu zama za Zlatko Krmpotic na sasa ni zama za Nasreddine Nabi.

 

Nyota huyo amesema: “Bado naona kwamba sijafikia pale ambapo nahitaji kufika, kiwango changu sawa ni kizuri lakini ninaona kabisa bado nina kazi ya kufanya kufikia pale ambapo ninapataka na inawezekana.

 

“Nadhani mwanzo wapo ambao walikuwa hawaniamini, ila kwenye mpira ninaamini kwamba juhudi na kumtanguliza Mungu ni vitu muhimu.”

Kwa sasa nyota huyo yupo nje ya dimba kwa kuwa aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba, na anatarajiwa kupelekwa Tunisia kwa ajili ya matibabu zaidi.

 

Kwenye ligi Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 yeye amecheza mechi nane na kuyeyusha dakika 587 katika mabao 20 ambayo wamefunga yeye ametoa pasi moja ya bao.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply