The House of Favourite Newspapers

Kidato cha Pili Kuanza Mitihani wa Kitaifa Leo

0


Wanafunzi wa kidato cha pili wapatao  646,148 kote nchini  wanatarajia kuanza Mitihani hiyo leo Jumatatu, Novemba 9, 2020 hadi Novemba 20, 2020 ambapo kati yao 301,831 (46.71%) ni Wavulana huku 344,317 (53.29%) wakiwa Wasichana.

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema idadi hiyo ni ongezeko la 5.7% ikilinganishwa na waliofanya mitihani hiyo mwaka jana.

 

Aidha, ameeleza kuwa Mitihani ya Darasa la Nne itafanyika Novemba 25 na 26, ambapo idadi ya Wanafunzi waliosajiliwa ni 1,825,679 wakiwemo Wavulana 909,068 na Wasichana 916,611.

Leave A Reply