The House of Favourite Newspapers

Kidunda: Nitafanya Vitendo Kesho, Katompa Atamba

0

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania’JWTZ’, Sajenti Seleman Kidunda amemtahadharisha mpinzani wake Tshimanga Katompa kuwa amejiandaa kufanya kwa vitendo na siyo kueleta maneno mengi wakati mpinzani wake amedai kutumwa na Jeshi la DR Congo kumsaka Askari wa Tanzania aliyepotea njia.

 

Kidunda na Katompa wanatarajia kupanda ulingoni kesho Jumapili katika pambano pambano la Usiku wa Mabingwa III ambalo litakuwa la ubingwa wa Dunia wa WBF litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar huku likidhaminiwa na Global Tv Online, Gazeti la Championi, Bongo Boxing Safari, Smart Gin, Wakala misitu TFS, JWTZ, Magadu Hotel Morogoro, Simba Courier, Suma JKT, Asas, Good Hope Lab, Kebbys Hotel, Clouds, Creative Bee, Kiboko Paints na SMH Logistics Coach.

Kidunda amewaambiwa Watanzania kabla ya kupima kuwa yeye kwa upande wake hana manano mengi kwa kuwa amejipanga kufanya vitendo kesho huku akisisita kwamba atakavyokuja ndivyo atakavyompokea ndani ya ulingo.

 

Kwa upande wa Katompa amefunguka yeye ameagizwa na mkuu wa majeshi ya DR Congo kumsaka Askari wa Tanzania aliyepotea njia hivyo kesho ataona balaa lake.

Mabondia wengine watakaopambana kesho ambao wamepima uzito ni Ismai Galiatano dhidi ya Denis Mwale, Ibrahim Class atazichapa na Israel Kamwamba, George Bonalacha ataminyama na Hassan Milanzi, Paul Magesta atapigana na Oscar Richard na Viguli Shafii dhidi ya Ally Kilongola.

 

Wengine ni Hamis Kibodi atacheza na Iddy Jumanne, Grace Mwakamela atacheza na Ruth Chisale, Najma Isike watapimana nguvu na Leila Yazidu na Daniel Materu dhidi ya Haruna Swanga.

Leave A Reply