The House of Favourite Newspapers

Arnorld Schwarzenegger Awajengea Nyumba Wanajeshi Wastaafu

0

MCHEZAJI filamu mkongwe na Gavana wa zamani wa Jimbo la California, nchini Marekani Arnorld Schwarzenegger amechangia dola 250,000 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 500 za Kibongo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 25 za wanajeshi wastaafu wasiokuwa na makazi nchini Marekani.

 

Nyumba hizo zenye chumba kimoja na sehemu kwa ajili ya joto, zitagawiwa kwa wanajeshi wastaafu waliopo mitaani California, ambao hawana makazi.

 

Tatizo la wanajeshi wastaafu kukosa makazi siyo jambo geni nchini Marekani, Baada ya Schwarzenegger kutoa msaada huo ambao ameita zawadi ya Christmasi, watu na mashirika mbalimbali yamejitokeza kusaidia wanajeshi wastaafu wasiokuwa na makazi nchini humo.

Movie gani ya Arnold Schwarzenegger unaikubali sana?

Leave A Reply