The House of Favourite Newspapers

Kifo cha Kanumba, Lulu Akutwa na kesi ya Kujibu – Video

0

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemkuta muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ana kesi ya kujibu katika tuhuma zinazomkabili za kumuua aliyekuwa staa wa Bongo Movie, Steven Kanumba bila kukusudia.

Mapema leo, Mahakamani hapo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Binadamu wa Hospitali ya Muhimbili, alitoa ushahidi wake akiilezea mahakama namna alivyopokea order ya Jeshi la Polisi kumtaka aufanyie uchunguzi mwili wa Kanumba ambapo baada ya kupasua ubongo walikuta mishipa midogo ya damu ikiwa imevujilia kwenye ubongo huku kisogoni kukiwa kumeganda damu.

Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa fani hiyo, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amesema baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa kuita mashahidi wanne amejiridhisha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.
Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa atajitetea chini ya kiapo na ameomba muda kwa ajili ya kufanya maandalizi.

Baadaye leo ataanza kujitetea mahakamani hapo.

NA RICHARD BUKOS | GPL

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

==

LULU AMWAGA CHOZI MAHAKAMANI! Alichokiona Daktari Kwenye Ubongo wa Kanumba!

Leave A Reply