The House of Favourite Newspapers

Kifo Cha Utata Arusha: Mrembo Akutwa Mwili Ukitoka Damu Kila Sehemu Aliitwa Na Mwenzake Usiku – Video

0

Mrembo aliyejulikana kwa jina la Mariam Bruno (34) mkazi wa Mtaa wa Olkereian Kata ya Olasiti Jijini Arusha amefariki Dunia katika mazingira ya Kutatanisha baada ya siku ya jumatatu kupigiwa simu na rafiki yake aitwaye Anitha amfuate maeneo ya baa ya Amarula iliyopo mtaa wa kambi ya Fisi kata ya Ngarenaro ambapo kuanzia hapo hakuwasiliana tena na ndugu zake mpaka pale walipopigiwa simu na polisi kwamba binti huyo amefariki yuko mochwari.

Ndugu hao wameelezwa kuwa Mariam alikosa hewa katika moja ya chumba katika baa hiyo jambo ambalo wameomba upelelezi kufanyika kwa haki ili kujua chanzo huku wakilalamika kuwa aliyempigia simu siku hiyo rafki yake huyo yuko mtaani na hajakamatwa bado na wamesema kuwa hawatazika mpaka wapate ukweli wa tukio zima.

Leave A Reply