The House of Favourite Newspapers

KIGOGO Amshika Pabaya Mbunge Mlinga – Video

0

MBUNGE wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mtu anayejiita KIGOGO katika mitandao ya kijamii kutumia namba ya simu ya mbunge huyo kuwalaghai watu kupitia mitandao ya kijamii.

 

Mlinga ameeleza hayo leo Mei 28, 2020, wakati akizungumza na +255 Global Radio kupitia kipindi cha Front Page.

 

“Huyu mtu anayejiita KIGOGO huko mitandaoni amechukua namba yangu ya simu na kuichapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kisha kuwaambia wanaomtafuta wampate kwa namba hiyo, nimepokea simu nyingi na meseji zaidi ya 600 ndani ya saa moja, watu wakinitukana na wengine kunipongeza. Nimeripoti polisi wanaendelea na uchunguzi.

 

“KIGOGO ni kikundi cha watu kwa sababu wanaposti kila baada ya dakika 10 au 15, na wanaposti taarifa mbalimbali kutoka maeneo tofauti. Imekuwa kawaida yao kuchukua namba za wabunge na kuziweka kwenye mtandao wao wakijifanya wao ndiyo mbunge huyo.

 

“Haya mambo ni ya kishamba sana, yanashusha hadhi ya nchi yetu, ni wakati sasa vyombo vya ulinzi na usalama vikawekeza kwenye mitandao kuwashughulikia watu hawa wanaoharibu image ya taifa letu. Mimi kama mlinga hawanichafui kwa lolote lakini wanaharibu taswira ya taifa letu, ” -amesema.

 

Leave A Reply