The House of Favourite Newspapers

Kigogo Jeshi la Polisi Auawa

0

WATU wasiojulikana nchini Nigeria wamempiga risasi na kumuua mmoja wa vigogo wa jeshi la nchi hiyo, Meja Jenerali Hassan Ahmed.

 

Meja Jenerali Ahmed aliuawa usiku wa Alhamisi nje kidogo ya Abuja wakati gari lake liliposhambuliwa kwa risasi, akitokea jijini Lokoja kwenda Abuja, akiwa na familia yake.

 

Dereva aliyekuwa anaendesha alijeruhiwa na mwanamke mmoja aliyekuwepo kwenye gari hiyo anayetajwa kuwa dada wa meja huyo, Safina Ahmed alitekwa.

Jeshi la nchi hiyo limeyaelezea mauaji hayo ni ‘tukio la kusikitisha’, huku kuuawa kwake kukiongeza hofu ya usalama nchini humo.

 

Meja Jenerali Ahmed hivi karibuni aliteuliwa na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo kuwa Mkurugenzi wa jeshi makao makuu. Haijajulikana mara moja kina nani hasa walio nyuma ya shambulio hilo na lina lengo gani hasa.

 

Kwa muda sasa nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya kiusalama ambapo makundi mbali mbali yenye silaha yamekuwa yakiendesha mauaji na utekaji wakilengwa raia na wanajeshi. Kutokana na vitendo hivyo Mamlaka nchini humo zimekuwa zikitupiwa lawama kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

 

Leave A Reply