The House of Favourite Newspapers

Kiiza ,Juuko wapata warithi Simba

0

KIIZA DIEGOHamisi Kiiza

 

Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
SIMBA sasa iko ‘siriaz’ katika kuhakikisha inafuta aibu ya kila mwaka baada ya kuamua kusajili wachezaji wa kazi ili msimu ujao uwe wa kazi kweli.

Wachezaji watatu, wawili raia wa Cameroon na mmoja kutoka Ivory Coast ambao wanaaminika watakuwa warithi wa Hamisi Kiiza, Juuko Murshid na Justice Majabvi, wanatarajiwa kutua nchini Jumamosi ijayo tayari kufanya majaribio.

juukoJuuko Murshid

Simba imeamua kuwaacha baadhi ya wachezaji wake kutokana na utovu wa nidhamu pamoja na kuwa na maneno ya chinichini yanayoua morali ya timu.
Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia  Hans Poppe amesema Majabvi ameomba kuondoka aende Australia kuishi na mkewe ambaye amepata kazi nchini humo.

“Kocha Mayanja atawaangalia na kujua kama kweli wanastahili kusajiliwa au la, hili tayari limeanza kufanyiwa kazi na kuna kampuni ambayo wako chini yao ndiyo itakayowaleta,” kilieleza chanzo.
Hans Poppe alipoulizwa kuhusiana na hilo, alisema:
“Kweli tuna wachezaji kadhaa ambao watafanyiwa majaribio, wako kutoka Magharibi mwa Afrika na kwingineko, ingawa sasa ni mapema mno.”
Wachezaji hao ni Patrick Wafo Ghomsi raia wa Cameroon mwenye uwezo wa kucheza vizuri nafasi ya kiungo. Huyu aliwahi kucheza Etoile du Sahel ya Tunisia, lakini sasa yuko Canon Younde ya Cameroon ambayo ni moja ya timu kubwa za nchini humo.

Mwingine ni Kiungo mkabaji Ouattara Abdoul Kader raia wa Cameroon, huyu anamaliza mkataba wake na Al Ahly Shandy ya Sudan na anaaminika mmoja wa viungo wababe, wakatili na anayecheza ‘kazikazi’.
Ukiachana na huyo, mwingine ni Morisane Sangare raia wa Ivory Coast aliwahi kucheza na kipa wa sasa wa Simba, Vincent Angban wakiwa Asec Mimosa, klabu ambayo imekuza wachezaji wengi wakiwemo akina Yaya Toure.

Mayanja atapata nafasi ya kuwaona wachezaji hao, ingawa itakuwa ligi ndiyo imemalizika.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply