The House of Favourite Newspapers

KIKI YA JAY Z, BEYONCE NI HATARI

SI Bongo tu, inaonekana kwa sasa kwenye ulimwengu wa burudani duniani kote mambo bila kiki hayaendi, wanamuziki, waigizaji na watu mbalimbali imefika hatua wapo tayari kufanya lolote lile ili mradi kuweka ‘attention’ kwenye jambo wanalotaka kulifanikisha.

 

Bila shaka, kwa wapenzi wa burudani watakuwa wanafahamu hapa Bongo, kiki mbalimbali zimefanyika na zinaendelea kufanyika kwa ajili ya kubusti kazi za wasanii na watu wamekuwa wakitokwa mapovu lakini ndiyo hivyo tena dunia ishafika huko na hakuna namna ya kubadilisha hali halisi.

Tukizungumzia kiki kwa Bongo hatuwezi kuzimaliza, zipo nyingi ambazo zimewahi kufanyika na kubamba lakini baadaye inabainika kwamba hakuna ukweli na wahusika walikuwa wanataka kupitisha jambo fulani.

 

Kwa mfano kiki ya hivi karibuni ilikuwa ni kusambaa kwa picha za Mtangazaji wa Clouds TV, Mwijaku akionekana amefunga ndoa na mrembo Nicole Franklyn, kumbe ulikuwa ni wimbo wa Mrisho Mpoto uitwao Nimwage Radhi.

Sasa kama kiki za Kibongo zinakushangaza cheki hii ya Jay Z na Beyonce. Wawili hawa ambao ni wanandoa wiki hii wameingia kwenye ‘headlines’ za showbiz, baada ya kuvujisha picha zao za utupu.

 

Iliwashangaza wengi, si kawaida kwa Jay Z na Beyonce kufanya jambo kama hilo, mara zote hasa Jay Z, ameonekana ni mtu makini na anayejiheshimu sana maana hata baada ya picha hizo kuvuja maswali ya watu wengi mitandaoni ilikuwa ni kwa nini Jay Z ameamua kufanya hivyo? Nini hasa kimemsukuma kushirikiana na mkewe kuachia picha za kuwadharirisha?

 

Wasanii Bongo watokwa mapovu

Baada ya tukio hilo la picha za wawili hao za utupu kusambaa baadhi ya wanamuziki Bongo walionyesha hisia zao juu ya tukio hilo wengine wakidai kwamba Jay Z na Beyonce hawakupaswa kufanya hivyo kwa sababu ni wanandoa.

Baadhi ya wanamuziki hao alikuwa ni Ibrahimu Mussa ‘R.O.M.A’, ambaye aliandika kwenye status yake ya Mtandao wa WhatsApp, kwamba Jay Z kajiangusha na kawadharirisha wanamuziki wa HipHop.

 

Kala Jeremiah, naye alikuwa na maoni yake ambapo alisema kwamba; “Nimeshan-gazwa na kilichotokea kiukweli, siamini kama Jay Z, ndiye kafanya hivyo. Ni jambo la kushangaza mno!”

Unataka kusikia na nini alisema George Mdemu ‘G Nako’? Yeye alisema kwamba kiki zimevuka mipaka kama wanandoa wapo tayari kudharirishana ili wafanikishe jambo lao basi muziki unaelekea pabaya sana.

 

Kwa nini Jay Z na Beyonce wamefanya hivyo?

Ndilo swali la watu wengi. Jibu ni kwamba wawili hao wameamua kutoa kali hiyo ya kuvujisha picha hizo za utupu kwenye kitabu chao chenye ratiba ya ziara yao ya shoo ambayo wameianza jana (Juma-tano), ili kuweka atensheni kwenye ziara hiyo itakayomalizika mwezi Oktoba.

 

Ziara

nyenyewe ni hii. Juni 13 (jana), walitarajiwa kuwa jijini Manchester, Uingereza kwenye Uwanja wa Etihad, Juni 15 watakuwa jijini London, huku Juni 19, wakipaa mpaka jijini Amsterdam, Uholanzi kwenye Uwanja wa NL Amsterdam Arena, kwa ajili ya makamuziki.

Juni 23 watakuwa jijini Copenhagen, kwenye Uwanja wa DK Parken, Juni 25 watakuwa Stockholm, kwenye Uwanja wa SW Friends Arena na Juni 28, watakuwa jijini Berlin, Ujerumani kwenye Uwanja wa DE Olympiastadion.

 

Wawili hao hawataishia hapo, watapiga shoo pia kwenye miji ya Warsaw, Cologne, Milan, Rome, Barcelona, Paris, Nice, Cleveland, Washington DC, Philadelphia, E. Rutherford, Boston, Minneapolis, Chicago, Detroit, Columbus, Nashville, Atlanta, Orlando, Miami, Arlington, New Orleans, Houston na Phoenix.

Makamuzi yataendelea pia kwenye miji ya Los Angeles, San Diego, Santa Clara, Vancouver na shoo yao ya mwisho itakuwa ni Oktoba 4, jijini Seattle kwenye Uwanja wa CenturyLink.

 

BONIPHACE NGUMIJE

MOBETO: NYUMBA TUNAYOISHI IMETOKA KWA DIAMOND – VIDEO

Comments are closed.