RAIS Mstafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza waombolezaji waliofika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kupumzisha mwili wa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Upendo Msuya aliyefariki dunia hivi karibuni.
Mamia ya waombolezaji walijitokeza kwenye mazishi hayo wakati wa kuupumzisha mwili wa Msuya kwenye nyumba yake ya milele ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi na Spika Mstaafu Anne Makinda walijumuika kumsindikiza.
JajiĀ Msuya alifariki Jumatano, Julai 19 akiwa katika Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.
Misa ya kumuaga marehemu ilifanyika katika Kanisa la KKKT Wazo leo Jumamosi asubuhi kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Marehemu ameacha watoto wanne.
NA DEINIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS