
RAIS Mstaafu, Jakaya Kikwete, alikuwa miongoni mwa waombolezaji wengi waliofika kutoa pole katika msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, aliyefariki jana Desemba 6 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Msiba huo unafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza-Makaburini jijini Dar es Salaam.

Akiongea msibani hapo mdogo wa marehemu, Allen Bendera, amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa Korogwe mkoani Tanga siku ya Jumapili ambapo taratibu za kumuaga jijini Dar es Salaam zinatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Lugalo jijini Dar na baadaye mwili kusafirishwa kuelekea mkoani Tanga.

Katika msiba huo, viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa wamefika nyumbani hapo kutoa pole.



NA DENIS MTIMA/GPL


Comments are closed.